Tuesday, March 14, 2017

RATIBA NUSU FAINALI FA CUP.

KLABU ya Chelsea mepangwa kucheza na mahasimu wao kutoka London Tottenham Hotspurs katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA. Arsenal ambao wanatarajia kuweka rekodi kwa kucheza nusu fainali yao ya 29 ya michuano hiyo, wao watapambana na Manchester City. Mechi zote mbili za nusu fainali zitachezwa katika Uwanja wa Wembley mwishoni mwa wiki inayoangukia Aprili 22 na 23 mwaka huu. Chelsea waliwang’oa Manchester United kwa kuifunga bao 1-0 jana, huku Spurs wakiitoa timu ya daraja la kwanza ya Millwall Jumapili iliyopita. Arsenal wao ambao ni mabingwa wa mwaka 2014 na 2015 katika michuano hiyo, waliwatoa Loncoln City Jumamosi iliyopita huku City nao wakiingia hatua hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka minne kwa kuichapa Middlesbrough mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment