Friday, March 31, 2017

CHUNG KUKATA RUFANI CAS.

MAKAMU wa rais wa wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Chung Mong-joon anatarajia kukata rufani kwenye Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS kupinga adhabu ya kufungiwa miaka mitano aliyopewa. Chung raia wa Korea Kusini ambaye alikuwa makamu wa rais wa FIFA kuanzia mwaka 1994 mpaka 2011, alikutwa na hatia mwaka 2015 ya kukiuka maadili ya shirikisho hilo wakati Korea Kusini ikitafuta nafasi ya uenyeji wa Kombe la Dunia 2022 miaka saba iliyopita, ambapo Qatar ndio waliopewa uenyeji. Chung anatarajiwa kuzungumzia uamuzi wake huo wa kukata rufani CAS Alhamisi ijayo jijini Seoul. Mapema kamati ya rufani ya FIFA ilipunguza adhabu ya Chung kutoka miaka sita aliyofungiwa awali mpaka mitano, wakitoa sababu kuwa hakukua na ushahidi wa kutosha wa kuvunjwa kwa kanuni hiyo. Mbali na adhabu hiyo ya kufungiwa kujishughulisha na masuala ya michezo, Chung pia alilimwa faini ya dola 49, 940.

No comments:

Post a Comment