Friday, March 24, 2017

DELE ALLI AFUNGIWA MECHI TATU NA UEFA.

KIUNGO wa Tottenham Hotspurs, Dele Alli amefungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa Europa League dhidi ya Gent. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza, alitolewa nje kwa kosa la kumkwatua Brercht Dejaegere wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa hatua ya 32 bora dhidi ya klabu hiyo ya Ubelgiji. Wakati timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1, Alli alimkwatua mwenye goti Dejaegere na kumuacha mwamuzi wa mchezo huo Manuel de Sousa bila chaguo zaidi ya kumpa kadi nyekundu. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 na kuwafanya Spurs kutolewa nje ya mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2. Pamoja na kutolewa Alli atalazimika kuitumikia adhabu yake ya kutocheza mechi katika michuano ijayo ya Ulaya ya vilabu kama Spurs wakifanikiwa kufuzu.

No comments:

Post a Comment