Friday, March 24, 2017

NAJUTA KUTOCHEZA NA RONALDO - TOTTI.

NGULI wa soka wa AS Roma, Francesco Totti amebainisha kuwa utambulisho wake wa kuwa mtu wa klabu moja uliingia katika tishio wakati Real Madrid walipomuwania na anajuta kutocheza sambamba na nguli wa Brazil Ronaldo De Lima. Totti mwenye umri wa miaka 40 ametumia kipindi cake chote cha soka kucheza kwenye klabu hiyo inayotoka katika mji mkuu wa Italia Rome, akicheza karibu mechi 800 kwa kipindi chote. Hata hivyo, aliwahi kupata nafasi ya kwenda kutafuta changamoto nyingine mpya wakati wakiwa kwenye kiwango juu huku Madrid ikiwa timu mojawapo iliyomuwania. Akizungumza wakati wa mahojiano nchini Italia, Totti amesema miaka mingi iliyopita alikaribia kujiunga na Madrid lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na heshima kubwa aliyokuwa nayo kwa mashabiki wa Roma. Totti aliendelea kudai kuwa kikubwa anachojutia ni kushindwa kucheza na Ronaldo pamoja na kutotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Roma.

No comments:

Post a Comment