Friday, March 17, 2017

GENK YA SAMATTA KUCHEZA NA CELTA VIGO EUROPA LEAGUE.

KLABU ya Genk ya Ubelgiji anayocheza nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta imepangwa kucheza na Celta Vigo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League. Genk ilitinga hatua hiyo kwa kishindo baada ya kuwagaragaza Wabelgiji wenzao Gent kwa jumla ya mabao 6-3, huku Samatta akifunga mabao mawili katika mchezo wa mkondo wa kwanza walioshinda mabao 5-2. Katika hatua nyingine Manchester United wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo wao wamepangwa kucheza na Anderlecht ya Ubelgiji huku Olympique Lyon wakicheza na Besiktas na Ajax Amsterdam wakipepetana na Schalke 04. Mechi za mkondo wa kwanza zinatarajiwa kuchezwa Aprili 13 huku zile za marudiano zikifuatia wiki moja baadae.

No comments:

Post a Comment