Friday, March 17, 2017

MADRID KUWAVAA WABABE WA ARSENAL ULAYA.

MABINGWA watetezi Real Madrid wanatarajia kupambana na Bayen Munich, wakati Barcelona wakipangwa kucheza na Juventus katika ratiba ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa upande mwingine mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza Leicester City wao wamepangwa kuchuana na Atletico Madrid huku Borussia Dortmund wakipepetana na AS Monaco waliotinga hatua hiyo baada ya kuitoa Manchester City katika 16 bora. Madrid ambao walitinga hatua hiyo baada ya kuitoa AS Napoli watakabiliwa na kibarua kizito mbele ya Bayern iliyoifurumusha Arsenal kwa jumla ya mabao 10-2 katika mechi mbili walizokutana. Kwa upande wa Barcelona wanaweza mwaka hu unaweza kuwa mzuri kwao kwani walitinga hatua hiyo kwa kuweka historia ya kipekee ya kutoka nyuma wakiwa wamefungwa mabao 4-0 na kutinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa mabao 6-1. Juventus kwa upande wao waliitoa FC Porto kwa jumla ya mabao 3-0 wakati Leicester walijiwekea historia ya kutinga hatua hiyo kwa kuiondosha Sevilla. Mechi za mkondo wa kwanza zinatarajiwa kuchezwa Aprili 11 na 12 huku zile za marudiano zikipangwa Aprili 18 na 19.

No comments:

Post a Comment