Tuesday, March 21, 2017

SCHWEINSTEIGER ATIMKIA MAREKANI.

KLABU ya Manchester United, imekubali kumuacha Bastian Schweinsteiger kujiunga na timu ya Chicago Fire inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Marekani-MLS. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo. Katika taarifa yake, Schweinsteiger amesema siku zote amekuwa akiangalia nafasi ambayo anaweza kufanya kitu cha kusaidia na kutengeneza kitu kikubwa ndio maana ameamua kwenda Chicago Fire. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na mshindi wa Kombe la Dunia alikuwa akifanya mazoezi mwenyewe na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 23 akiwa United baada ya Jose Mourinho kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kiangazi mwaka jana. Hata hivyo, alirejea katika kikosi cha kwanza kabla ya mchezo wa Europa League dhidi ya Fenernahce Novemba mwaka jana na kucheza mechi yake ya kwanza kweney mchezo wa Kombe la EFL dhidi ya West Ham United.

No comments:

Post a Comment