Tuesday, March 21, 2017

VARDY ADAI KUPOKEA VITISHO VYA KUUAWA.

MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Jamie Vardy amesema amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa na familia yake ikilengwa toka meneja Claudio Ranieri alipotimuliwa. Nyota huyo mwneye umri wa miaka 30 analaumu tuhuma mbaya na za uongo kuwa ndiye aliyelazimisha klabu hiyo kufikia uamuzi wa kumtimua meneja huyo raia wa Italia. Ranmieri aliondoka Febrauri, miezi tisa baada ya kushinda taji la Ligi Kuu, huku klabu ikiw nafasi ya 17 katika msimamo ambapo nafasi yake ilishikiliwa na msaidizi wake Craig Shakespeare. Akizungumza na wahabari, Vardy amesema ni jambo linalotisha kwani alisoma habari moja kuwa alikuwepo katika mkutano baada ya mechi dhidi ya Sevilla na kushinikiza kutimuliwa kwa Ranieri. Vardy aliendelea kudai kuwa anasikitika kwasababu hakuwepo katika kikao hicho na hakuhusika na chochote katika uamuzi wa klabu uliochukua.

No comments:

Post a Comment