Tuesday, March 21, 2017

RONALDO ATWAA TUZO NYINGINE.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2016 wa Ureno baada ya kuiongoza nchi yake kutwaa taji lao la kwanza la michuano ya Ulaya akiangazi mwaka jana. Ronaldo aliwashinda mchezaji mwenzake wa Madrid Pepe na kipa wa Sporting Lisbon Rui Patricio katika kinyang’anyiro hicho. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 aliiongoza Madrid kushinda taji lake la 11 la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei mwaka jana kwa kufunga penati ya ushindi dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid huku akimaliza kama mfungaji bora kwa mabao yake 16. Ingawa Ronaldo aliumia mapema katika mchezo wa fainali ya michuano ya Ulata dhidi ya wenyeji Ufaransa, Ureno ilijitutumua na kushinda mchezo huo kwenye dakika za nyongeza na kutwaa taji lao la kwanza kubwa katika historia. Akizungumza na wanahabari, Ronaldo amesema umekuwa mwaka mzuri na muhimu kwasababu michuano ya Ulaya ndio ilikuwa pekee ambayo hajawahi kushinda.

No comments:

Post a Comment