Tuesday, March 21, 2017

RAIS MPYA CAF AANZA KUPUNGUZA VYEO ANAVYOSHIKILIA ILI KUKIDHI MASHARTI.

RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, Ahmad Ahmad amejizulu wadhifa wake kama makamu wa rais wa baraza la seneti nchini Madagascar. Ahmad ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Soka la Madagascar-MFF, aliachia wadhifa huo mapema jana baada ya kudumu toka Februari mwaka 2016. Ahmad mwenye umri wa miaka 57 na kocha wa zamani wa klabu ya AC Sotema, alipokelewa rasmi na maofisa wa MFF na jamii ya Kiislamu katika hoteli ya Carlton jijini Antananarivo ambako alihutubia waliohudhuria. Alhamisi iliyopita Ahmad alichaguliwa kuwa rais mpya wa CAF kwa kupata kura 34 dhidi ya 20 za rais aliyemaliza muda wake Issa Hayatou ambaye alikaa madarakani kwa kipindi cha miaka 29. Ahmad ambaye pia amewahi kushikilia nafasi ya uwaziri kwa vipindi viwili tofauti nchini kwake, pia anategemewa kuachia nafasi yake kama rais wa MFF kama sheria za CAF zinavyotaka.

No comments:

Post a Comment