Monday, March 27, 2017

KATIBU MKUU WA CAF ABWAGA MANYANGA.

KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, Hicham El Amrani amejiuzulu wadhifa wake huo jana, ikiwa imepita wiki moja baada ya rais aliyedumu kwa kipindi kirefu Issa Hayatou kushindwa kwenye uchaguzi na Ahmad Ahmad wa Madagascar. Katika barua yake ya kujiuzulu kwa CAF, El Amrani amesema ataondoka rasmi leo lakini hajatoa sababu zozote kwa uamuzi wake huo. El Amrani mwenye umri wa miaka 37 raia wa Morocco amekuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka sita iliyopita. Hayatou aliondolewa kwenye nafasi ya urais wa CAF siku 10 zilizopita katika uchaguzi uliofanyika huko Ethiopia, ambapo wajumbe sita wa kamati ya utendaji waliokuwa wakimuunga mkono kwenye uchaguzi huo nao pia walipoteza naafsi zao. Hayatou mwenye umri wa miaka 70 ameingoza CAF kwa kipindi cha miaka 29.

No comments:

Post a Comment