Monday, March 27, 2017

NIMETIMIZA NDOTO ZANGU KWA KUFUNDISHWA NA BABA - DALEY BLIND.

BEKI wa kimataifa wa Uholanzi na Manchester United, Daley Blind amesema kucheza chini ya baba yake Danny ilikuwa ni moja ya ndoto zake pamoja na kocha huyo wa timu ya taifa ya nchi hiyo kutimuliwa. Uholanzi chini Danny Blind ilijikuta ikitandikwa mabao 2-0 na Bulgaria Jumamosi iliyopita na kuiacha nchi hiyo kwenye hatari ya kutofuzu michuano mikubwa kwa mara ya pili mfululizo. Blind mwenye umri wa miaka 55 alichukua nafasi ya Guus Hiddink mwaka 2015 lakini alishindwa kuiwezesha nchi hiyo kufuzu michuano ya Ulaya iliyofanyika nchini Ufaransa kiangazi mwaka jana. Fred Grim ndio anatarajiwa kuchukua mikoba ya muda wakati Uholanzi itakapovaana na Italia kesho. Akizungumza na wanahabari kuhusu kutimuliwa kwa baba yake, Daley amesema kufanya kazi naye katika viwango vya juu ilikuwa ndoto yake kubwa na imetimia hivyo anajivunia.

No comments:

Post a Comment