Tuesday, March 28, 2017

MAN CITY WALIMWA ADHABU.

KLABU ya Manchester City imelimwa faini ya paundi 35,000 na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake kwenye mchezo wa Liverpool mwezi huu. City walikubali kosa wiki iliyopita baada ya wachezaji kadhaa kupingwa penati waliyopewa Liverpool kwenye mchezo huo uliofanyika Machi 19. Wachezaji hao waliendelea kulalamika hata baada ya James Milner kufunga penati hiyo kwa Liverpool iliyowapa uongozi kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1. Katika taarifa yake FA ilidai baada ya tume huru ya kisheria kusikiliza kesi hiyo iliamua kutoa uamuzi wa kuilima faini kufuatia klabu hiyo kukiri kufanya makosa hayo.

No comments:

Post a Comment