Tuesday, March 28, 2017

UWANJA WA KINA TEVEZ WAWAKA MOTO.

UWANJA wa klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki Ligi Kuu ya China wa Hongkou umeharibiwa vibaya kufuatia kuungua moto. Hakuna majeruhi wowote walioripotiwa kufuatia tukio hilo lililotokea mapema leo asubuhi. Taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo zinadai kuwa moto haukuathiri majukwaa au sehemu ya kuchezea na uchunguzi unaendelea kufanyika kubaini chanzo chake. Klabu hiyo inayonolewa na Gus Poyet, ilimsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Carlos Tevez mwaka jana kwa kitita cha paundi milioni 40. Pia kikosi cha timu hiyo kinajumuisha nyota wengine wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwemo Demba ban a Obafemi Martin. Ligi Kuu ya China imeanza rasmi mapema mwezi huu huku Shenhua ikitarajiwa kucheza mechi yake inayofuata nyumbani dhidi ya Changhun Yatai Jumapili ya Aprili 16 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment