Friday, March 31, 2017

SCHNNEIDERLIN KUIKOSA LIVERPOOL.


KIUNGO wa Everton, Morgan Schneiderlin anatarajiwa kuukosa mchezo wa derby ya kesho dhidi ya Liverpool na pia safari ya kwenda kucheza na Manchester United wiki ijayo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya kigimbi aliyopata kwneye mchezo dhidi ya Hull City machi 18 mwaka huu lakini mapema wiki hii alionekana akifanya mazoezi mepesi gym. Hata hivyo, meneja wa Everton Ronaldo Koeman amesema Schneiderlin hataweza kucheza mechi hiyo ya kesho huku pia akiongeza anaweza asiwe fiti kwenye mchezo ujao dhidi ya United Jumanne ijayo. Koeman aliendelea kudai kuwa pamoja na nyota huyo kuanza mazoezi mepesi lakini hadhani kama atakuwepo kwenye mechi wala ile ya Jumanne ila anamtegemea atakuwa fiti kwa ajili ya mechi dhidi ya Leicester City. Taarifa hizo ni pigo kubwa kwa Everton wenye matumaini ya kushinda derby yao ya kwanza katika Ligi Kuu toka mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment