Friday, April 21, 2017

BARCELONA KUIKATIA RUFANI ADHABU YA NEYMAR.


KLABU ya Barcelona inatarajiwa kwenda kukata rufani katika Mahakama Maalumu ya Michezo nchini Hispania-TAD, katika jitihada zao za kujaribu kupunguza adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyopea Neymar kuelekea mchezo wao wa Clasico. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alitolewa nje kwa kupewa kadi mbili za njano katika mchezo wa dhidi ya Malaga, kabla ya kuongezewa adhabu ya mechi tatu na Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Kawaida kadi mbili za njano alizopewa alitakiwa kukosa mechi moja lakini kutokana na na kumshambulia mwamuzi kwa maneno wakati alipopewa kadi nyekundu ndio kulikofanya aongezewe adhabu. Baada ya kukata rufani ya kwanza na kukataliwa Barcelona sasa wameamua kusogea mbele zaidi kwa kwenda TAD ili kujaribu kumpigania nyota wao huyo awepo katika mchezo huo wa Clasico dhidi ya mahasimu wao Real Madrid Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment