Friday, April 21, 2017

RATIBA ZA NUSU FAINALI CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE.

RATIBA ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepangwa baada ya kukamilika kwa hatua ya robo fainali na kupatikana timu nne zilizosonga mbele. Katika ratiba hiyo Real Madrid na majirani zao Atletico Madrid wamepangwa kucheza pamoja huku mchezo wa mkondo wa kwanza ukitarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Mechi nyingine katika ratiba hiyo itawakutanisha AS Monaco ambao wataanzia nyumbani kupambana na mabingwa wa Serie A Juventus. Mechi za mkondo wa kwanza zinatarajiwa kuchezwa Mei 2 na 3 huku zile za marudiano zikitarajiwa kuchezwa Mei 9 na 10.
 Pia Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA limepanga ratiba ya nusu fainali ya michuano ya Europa League ambapo Manchester United wataanzia ugenini kupambana na Celta Vigo huku Ajax Amsterdam wao wakipangwa kucheza na Olympique Lyon ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment