Friday, April 21, 2017

SABA WAFARIKI WAKIANGALIA MPIRA WA MANCHESTER.

WATU saba wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kupigwa shoti ya umeme wakati wakitazama mechi kati ya Manchester United ya Uingereza na Anderlecht ya Ubelgiji nchini Nigeria. Mashabiki wa soka walikuwa wamekusanyika kwenye kituo cha kutazama mechi kupitia runinga katika mji wa Calabar kusini mwa nchi hiyo mkasa ulipotokea. Manchester United walishinda 2-1 kwenye mechi hiyo ya hatua ya robo fainali ya Europa League. Polisi nchini Nigeria wamesema watu saba walifariki na wengine 10 wakajeruhiwa na wamelazwa hospitalini. Mwandishi mmoja nchini humo ameambia BBC kwamba kisa hicho kilitokea baada ya waya wa umeme kuangukia jumba.

No comments:

Post a Comment