Friday, April 28, 2017

BAYERN YAMUONGEZA MKATABA THIAGO ALCANTARA.

KLABU ya Bayern Munich imetangaza kumuongeza mkataba mpya kiungo wa kimataifa wa Hispania, Thiago Alcantara. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kusaini mkataba wa nyongeza ya miaka miwili ambao utamuweka Allianz Arena mpaka Juni mwaka 2021. Thiago alijiunga na Bayern akitokea Barcelona mwaka 2013 na kujiimarisha mpaka kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza pamoja na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara. Hata hivyo, msimu huu unaonekana kuwa mzuri kwake kwani ameshacheza mechi 39 za mashindano yote akifunga mabao nane na kusaidia mengine tisa. Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge amesema Thiago ni mmoja kati ya wachezaji wazuri na anafurahi kuendelea kuwepo naye.

No comments:

Post a Comment