Friday, April 28, 2017

LOVREN APEWA MKATABA MREFU LIVERPOOL.

BEKI wa kati wa Liverpool, Dejan Lovren amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo ambao unamalizika 2021. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 alitua Anfield akitokea Southampton kwa kitita cha paundi milioni 20 mwaka 2014 na mkataba wake wa sasa ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwakani. Beki huyo wa kimataifa wa Croatia alianza kwa kusuasua katika msimu wake wa kwanza lakini alifanikiwa kurejea kwenye kiwango chake na kuja kucheza mechi 105 akiwa na klabu hiyo huku akifunga mabao manne. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Lovren amesema anadhani ni mtu mwenye furaha zaidi duniani kwasasa. Lovren aliendelea kudai kuwa ilikuwa ni ndoto zake kubakia Liverpool kwa kipindi kirefu zaidi kwani anaipenda klabu hiyo. Lovren amecheza mechi 28 msimu huu na kufunga mabao mawili.

No comments:

Post a Comment