Friday, April 28, 2017

POGBA KUIKOSA SWANSEA CITY.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema Paul Pogba anatarajiwa kukosa mchezo wa Ligi Kuu Jumapili hii dhidi ya Swansea City utakaofanyika Old Trafford, lakini anatarajiwa kurejea tayari kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainalia ya Europa League Alhamisi ijayo. Pogba alitolewa nje kabla ya kumalizika kwa mchezo kati ya United dhidi ya Burnley Jumapili iliyopita kutokana na kupata majeruhi ya msuli wa nyuma ya paja na kumfanya kukosa mchezo wa jana waliotoka sare ya bila kufungana na mahasimu wao wa jiji Manchester City. Na Mourinho sasa amethibitisha kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa hatakuwepo katika mchezo huo dhidi ya Swansea mwishoni mwa wiki hii. Hata hivyo, Mourinho aliwaambia wanahabari kuwa Pogba atakuwepo katika mchezo dhidi ya Celta Vigo.

No comments:

Post a Comment