Friday, April 28, 2017

WENGER ASEMA BADO SANA KWA SPURS KUFIKIA HADHI YA ARSENAL.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema itawachukua zaidi ya miaka kadhaa kwa Tottenham Hotspurs kuendelea kupata mafanikio kabla ya kuweza kutajwa rasmi kwamba ndio watawala wa soka kaskazini mwa jiji la London. Kauli ya Wenger imekuja kufuatia mafanikio ambayo Spurs wameyapata msimu huu wakiwa wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakitofautiana alama nne na Chelsea. Ushindi kwa Spurs katika mchezo wao dhidi ya Arsenal utakaofanyika White Hart Lane Jumapili hii, utaihakikishia klabu hiyo kumaliza msimu wa ligi wakiwa juu ya Arsenal toka Wenger alipokuwa meneja mwaka 1996. Wakati huohuo, Wenger amesema Arsenal iliwahi kutaka kumsajili Dele Alli kabla ya kwenda Spurs. Wenger amesema maskauti wa Arsenal walikua wakimfuatilia toka akiwa kinda na Spurs walifanya vyema kumsajili kwani ni mchezaji aliyekamilika.

No comments:

Post a Comment