Friday, April 28, 2017

CONTE ADOKEZA KUREJEA SERIE A.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amedokeza kuwa angependa kupata nafasi ya kurejea ya Serie A siku zijazo. Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus, alitua Stamford Bridge mwaka jana na kuongoza vyema Chelsea ambayo iko kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la FA katika msimu wake wa kwanza. Hata hivyo, Conte amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea tena Italia mara kadhaa huku klabu ya Inter Milan ikitajwa kutaka kumnasa kocha huyo. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo, Conte amesema siku zote moyo wake umekuwa Italia na amekuwa akifahamu kuwa iko siku atarejea tena Serie A. Chelsea kwasasa ndio vinara wa ligi wakitofautiana alama nne na Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku wakiwa tayari wamefika hatua ya fainali ya Kombe la FA na watacheza dhidi ya Arsenal.

No comments:

Post a Comment