Friday, April 28, 2017

CELTA VIGO YATISHIA KUISHITAKI MAN UNITED.


KLABU ya Celta Vigo imetishia kuishitaki Manchester United katika Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kufuatia klabu hiyo kushindwa kuwapatia tiketi zao zote za mchezo wa mkondo wa nusu fainali ya Europa League utakaofanyika Old Trafford. Kwa mujibu wa kanuni za UEFA zinaeleza kuwa klabu mwenyeji inatakiwa kutoa asilimia ya tano ya sehemu ya uwanja kwa ajili ya mashabiki wa ugenini. Uwanja wa Old Trafford ndio uwanja mkubwa zaidi miongoni mwa klabu za Ligi Kuu ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki zaidi 75,000. Celta Vigo wamethibitisha kupokea tiketi 1,900 pekee kati ya 3,780 ambazo wanastahili kupatiwa kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika Mei 11 mwaka huu na juhudi za kujaribu kupatiwa ufafanuzi kuhusiana na hilo zimeshindikana. Msemaji wa Celta Vigo amesema kikao kilifanyika toka juzi kati ya pande zote mbili lakini hakuna chochote kilichotekelezwa mpaka sasa. Msemaji huyo aliendela kudai kuwa kama suala hilo lisipopatiwa ufumbuzi katika siku za karibuni ni wazi watalazimika kuiomba UEFA kuingilia kati.

No comments:

Post a Comment