KLABU ya Bayern Munich imetangaza kumsajili Kingsley Coman kwa mkataba wa moja kwa moja kutoka Juventus. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesaini mkataba wa mpaka Juni 2020 baada ya Bayern kukubali kulipa euro milioni 21 zilizokuwa zikihitajika. Mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amesema Coman ni mchezaji muhimu kwa ajili ya maendeleo ya baadae ya timu yao ndio maana wameamua kumsajili moja kwa moja. Coman alijiunga na Bayern kwa mkopo wa miaka miwili mwaka 2015 huku mabingwa hao wa Bundesliga wakiwa na nafasi ya kumsajili moja kwa moja kama wakimuhitaji. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, hivi karibuni alikuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Allianz Arena huku klabu za Ligi Kuu Chelsea na Manchester City zikitajwa kumuwania.
No comments:
Post a Comment