Thursday, April 27, 2017

BEKI WA ZAMANI WA CITY AMPONDA GUARDIOLA.

BEKI wa zamani wa Manchester City, Martin Demichelis amesema msimu wa kwanza wa meneja Pep Guardiola katika klabu hiyo unaonyesha jinsi gani mtangulizi wake Manuel Pellegrini alivyodharauliwa. Hali inavyokwenda kwasasa inaonyesha Guardiola anaweza kumaliza msimu wake wa kwanza bila taji kwa mara ya kwanza toka aanze kibarua hicho. Akizungumza na wanahabari, Demichelis amesema ukiangalia timu ya City hivi leo utaona ni jinsi gani hakuna kinachokuja kirahisi hata kwa kocha bora. Beki huyo aliendelea kudai kuwa kadri muda unavyokwenda kila mtu ataona na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na Pellegrini. Pellegrini alishinda taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo baada ya kujiunga nao akitokea Malaga Juni mwaka 2013. Meneja huyo pia alimaliza nyuma ya Chelsea kwenye mwaka wake wa pili uliofuatia na kuiongoza City katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya mkataba wake kumalizika kiangazi mwaka jana.

No comments:

Post a Comment