Thursday, April 27, 2017

SAKHO AIWEKA NJIA PANDA PALACE.

MENEJA wa Crystal Palace, Sam Allardyce ana matumaini Mamadou Sakho hajapata majeraha makubwa kwenye goti lake wakati walipofungwa nyumbani na Tottenham Hotspurs jana. Sakho alilazimika kutolewa nje baada ya kuumia kwa kukwatuliwa na mshambuliaji Spurs Harry Kane na beki huyo ambaye yuko kwa mkopo Palace amelazimika kufanyiwa vipimo zaidi kugundua ukubwa wa tatizo lake. Kutokana na mkataba wa mkopo wa Sakho kutoka Liverpool kukaribia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kuwa amecheza mechi yake ya mwisho Palace lakini Allardyce ana matumaini majeruhi hayo hayakuwa makubwa sana. Akizungumza na wanahabari, Allardyce amesema hafahamu ukubwa wa tatizo la Sakho lakini ana matumaini hayatakuwa makubwa sana mpaka kumfanya kukaa nje ya uwanja kwa msimu wote uliosalia.

No comments:

Post a Comment