Thursday, April 27, 2017

KOSCIELNY HATIHATI KUWEPO DHIDI YA SPURS.

KLABU ya Arsenal inaweza kumkosa beki wake mahiri Laurent Koscielny katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao wa London ya Kaskazini Tottenham Hotspurs Jumapili hii. Hatua hiyo inakuja kufuatia beki huyo kuumia goti katika mchezo wao jana walioshinda bao 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi Leicester City. Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo, Wenger amesema Koscielny amepata matatizo ya goti lakini hajui ameumia kwa kiasi gani mpaka atakapofanyiwa vipimo. Huku beki mwingine Shkodran Mustafi pia akiwa katika hatihati kutokana na majeruhi ya msuli, kukosekana kwa Koscielny kunaweza kuiathiri Arsenal kwa kiasi kikubwa haswa wakati huu ambao wanafukuzia nafasi nne za juu ili wafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Arsenal kwasasa wako nafasi ya sita katika msimamo wa ligi, na wanakwenda kupambana na Spurs ambao hawajafungwa mchezo wowote katika uwanja wao wa nyumbani.

No comments:

Post a Comment