Wednesday, April 26, 2017

FA YAMSTAAFISHA MAPEMA MTUKUTU BURTON.

KIUNGO wa Burnley, Joey Burton amesema kuwa atalazimika kustaafu soka mapema baada ya kulimwa adhabu ya kufungiwa miezi 18 na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa makosa ya kamari. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye pia ametozwa faini ya paundi 30,000, anatuhumiwa na FA kucheza kamari 1,260 katika kipindi cha miaka 10 kati ya Machi 2006 na Mei 2016. Barton ambaye amethibitisha nia yake ya kukata rufani kupinga ukubwa wa adhabu hiyo, amekubali kuwa alivunja sheria za FA lakini amedai chama hicho cha soka kimetoa adhabu kali mno na hawakuzingatia kuathirika kwake na kamari ambapo alipeleka mpaka taarifa za kupata msaada wa kitabibu. Katika taarifa yake aliyotoa kwenye tovuti yake, Burton amesema amesikitishw ana adhabu hiyo kali aliyopewa, jambo ambalo litamlazimu kustaafu mapema kucheza soka.

No comments:

Post a Comment