Saturday, April 29, 2017

TOURE AINANGA MAN UNITED.

KIUNGO mahiri wa Manchester City, Yaya Toure amesema kwa jinsi Manchester United walivyoshangilia sare ya bila kufungana na City inaonyesha jinsi gani klabu hiyo ilivyopiga hatua toka alipojiunga nao. City walitawala mchezo huo kwa kwa asilimia 69 na kupiga mashuti 19 kulinganisha na matatu ya ya United lakini walishindwa kabisa kumfunga kipa David de Gea. Matokeo hayo yanaifanya City kuendelea kukaa juu ya mahasimu wao na kumaanisha United bado wako nje ya eneo la kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Lakini mashabiki wa United walionekana kufurahia kwa kiasi kikubwa sare hiyo mara mchezo ulipomalizika na Toure amesema imekuwa tofauti na wakati anajiunga na City mwaka 2010 wakati Sir Alex Ferguson akiwa anatawala Ligi Kuu. Akizungumza na wanahabari, Toure amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa toka ametua hapo kwa kipindi cha nyuma United ndio walikuwa wakitawala hivyo kuona mashabiki wao wakishangilia sare inaonyesha jinsi gani walivyopiga hatua.

No comments:

Post a Comment