Monday, May 1, 2017

INTER MILAN KUMTENGEA OFA NONO SIMEONE.

KLABU ya Inter Milan inadaiwa kuandaa mkutano na kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ambapo watampa ofa rasmi na kujiunga na wakongwe hao wa soka la Italia. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika baada ya mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya mahasimu wao Real Madrid. Inter inatarajia kumpa ofa Simeone ya mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya euro milioni 6 kila msimu. Mkataba wa sasa wa Simone katika klabu hiyo unamalizika mwaka 2018 na bado hajazungumzia kuhusu kuongeza mwingine.

No comments:

Post a Comment