Monday, May 1, 2017

WENGER AWAPONGEZA SPURS.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amewapongeza Tottenham Hotspurs baada ya kushinda mchezo wao wa derby ya kaskazini mwa London katika Uwanja wa White Hart Lane kwa mabao 2-0 na kuwahakikishia nafasi ya kumaliza juu ya mahasimu wao hao kwa mara ya kwanza toka mwaka 1995. Mabao ya Delle Alli na Harry Kane aliyefunga kwa penati yalitosha kuwahakikishia ushindi Spurs huku nafasi ya Arsenal kumaliza kwenye nafasi nne za juu ikiwa mashakani. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Wenger aliwapongeza Spurs lakini aliongeza kuwa wakati wanaanza msimu malengo makubwa sio kumaliza juu ya mahasimu wao bal ni kushinda taji la ligi. Wenger aliendelea kudai kuwa wanasikitika kwa kuwa hawapo katika mbio za ubingwa haswa katika kipindi hiki wakati wa ligi ikielekea mwishoni.

No comments:

Post a Comment