Monday, May 1, 2017

NYOTA SABA WA UNITED KUIKOSA CELTA VIGO.

KLABU ya Manchester United inatarajiwa kwenda katika mchezo wao wa mkono wa kwanza wa nusu fainali ya Europa League Alhamisi hii bila nyota wake saba wa kikosi cha kwanza. Meneja wa United, Jose Mourinho alishuhudia orodha ya majeruhi katika kikosi chake ikiongezeka jana kufuatia sare ya bao 1-1 waliyopata nyumbani dhidi ya Swansea City ambapo mabeki wake Luke Shaw na Eric Bailly walitolewa nje. Kukosekana kwa Bailly kunamaanisha kuwa Mourinho hatakuwa na beki wa kati anayejulikana kufuatia Chris Smalling na Phil Jones na pia kuwa majeruhi. Lakini kiungo Juan Mata alirejea katika benchi la United kwenye mchezo huo dhidi ya Swansea baada ya kukosa mechi nane kutokana na matatizo ya nyonga. Paul Pogba naye pia anatarajiwa kurejea katika mchezo huo utakaofanyika nchini Hispania baada ya kukosa mechi mbili lakini Zlatan Ibrahimovic, marcos Rojo na Tomothy Fosu-Mensah hawatakuwepo.

No comments:

Post a Comment