Tuesday, May 2, 2017

TETESI ZA USAJILI KUTOKA MAJUU.


MAN UTD INAMTAKA BELOTTI
KLABU ya Manchester United inadaiwa kutaka kumuania mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti. United imekuwa ikihusishwa na taarifa za kutaka mshambuliaji mwenye jina kubwa kwa ajili ya msimu ujao, huku Antoine Griezmann akiongoza kwenye listi yao. United walio chini ya Jose Mourinho wanadaiwa kuwasiliana na klabu hiyo ya Serie A ili kuonyesha kuwa wanamfuatilia mashambuliaji huyo ambaye pia amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na Arsenal.

Source: ESPN


BARCA WAANZA MAZUNGUMZO YA BELLERIN
KLABU ya Barcelona inadaiwa kujiandaa rasmi kwa ajili ya kumsajili Hector Bellerin kutoka Arsenal. Barcelona wamemfanya beki huyo wa upande wa kulia kuwa chaguo lao namba moja katika usajili ujao wa kiangazi, huku klabu hiyo ikiunga mkono mipango ya katibu wa ufundi David Fernandez ya kujaribu kumrejesha nyota huyo Camp Nou. Hata hivyo, nyongeza ya mkataba mpya aliyopewa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 inamaanisha Barcelona watalazimika kutoka dau kubwa zaidi ili kuishawishi Arsenal kuamuachia.

Source: Mundo Deportivo


CHELSEA YAKARIBIA KUMNASA VAN DIJK
KLABU ya Chelsea inaamini ndio wanaongoza mbio za kumuwania kumsajili kiungo Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 25 kutoka Southmpton. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akiwaniwa na karibu kila klabu kubwa katika Ligi Kuu mwaka huu, lakini Chelsea wamedai kuwa ofa yao ya kumtoa beki wa kati Andreas Christensen ambaye yuko kwa mkopo Borussia Moenchengladbach kwenda Southampton itarahisisha dili lao.

Source: The Sun


ARSENAL KUONGEZA MKURUGENZI WA MICHEZOMKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Hoffenheim, Alexander Rosen anadaiwa kuongezwa katika orodha ya watu wanaoweza kuchukua nafasi hiyo mpya kwa klabu ya Arsenal. Mbali na Rosen wapo Marc Overmars na mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc ambao nao pia wanafikiriwa kwneye nafasi hiyo.

Source: Mirror


OZIL ANATAKA PAUNDI 300,000 KWA WIKI
KLABU ya Arsenal inadaiwa bado inasita kuimarisha ofa ya mkataba mpya wa Mesut Ozil kutokana na wasiwasi juu ya kujitoa kwa klabu kwa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. Taarifa zinadai kiungo huyo ambaye amekuwa akisuasua kiwango chake hivi karibuni amekataa kusaini ofa ya paundi 250,000 kwa wiki na badala yake anataka paundi 300,000 kwa wiki.

Source: Daily Mail


UNITED YAONGOZA MBIO ZA KUMSAJILI SCHMEICHEL
KLABU ya Manchester United inadaiwa kuwazidi majirani zao Man City katika mbio za kumsajili kipa wa Leicester City Kasper Schmeichel. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30, mtoto wa nguli wa zamani wa United Peter ndio anatajwa kuwa chaguo namba moja la kuziba nafasi ya David de Gea ambaye anategemewa kujiunga na Real Madrid majira ya kiangazi.

Source: Sky SportsNo comments:

Post a Comment