Tuesday, May 2, 2017

IBRAHIMOVIC ATAREJEA AKIWA IMARA ZAIDI - WAKALA.

WAKALA wa mchezaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola, amesema mshambuliaji huyo amefanyiwa upasuaji kwenye goti lake na kwamba umekuwa na mafanikio. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 35 aliumia kwenye kano za goti wakati wa mechi ya Europa League dhidi ya Anderlecht Aprili 20. Lakini Raiola amesema kwenye taarifa kwamba jeraha alilopata mchezaji huyo halitishii uchezaji wake. Ibrahimovic anakaribia kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja Old Trafford, na bado hajaafikiana na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. Mkongwe huyo amefunga mabao 28 msimu huu, baada ya kujiunga na United bila kulipiwa ada yoyote kutoka Paris Saint-Germain majira ya joto mwaka jana.

No comments:

Post a Comment