Tuesday, May 2, 2017

USHINDI WAMPA JEURI KLOPP.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amewataka wachezaji wake kuendelea kujituma zaidi baada ya kurejesha matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu kufuatia ushindi dhidi ya Watford. Bao pekee lililofungwa na Emre Can lilitosha kuwapa ushindi wa Liverpool na kuwafanya kuendelea kubaki katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwazidi Manchester City kwa alama tatu. Ushindi katika mechi tatu zijazo za Liverpool dhidi ya Southampton, West Ham United na Middlesbrough utakuwa umewahakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa ulaya msimu ujao. Hata hivyo, Klopp amedai bado kuna kazi kubwa ta kufanya kuhakikisha wanaendeleza umakini katika mechi zao zilizosalia.

No comments:

Post a Comment