Tuesday, May 2, 2017

WAKALA WA VERRATTI AITAKA PSG KUTOA MSIMAMO WAO KWA MTEJA WAKE.

WAKALA wa Marco Verratti ametaka kuitishwa kwa mazungumzo na Paris Saint-Germain juu ya mustakabali wa kiungo huyo baada ya fainali ya Coupe de France. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia ameendelea kuhusishwa na tetesi za kwenda Barcelona mwishoni mwa msimu huu kufuatia kutofanya vyema sana chini ya meneja Unai Emery. PSG tayari wameshashinda mataji mawili msimu huu lakini walitolewa na Barcelona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kuna dalili za kupoteza taji la Ligue 1 kwa Monaco. Wakala wa Verratti, Donato Di Campli, hataki kuharakisha sana mazungumzo lakini ameweka wazi anataka kuzungumza na klabu hiyo baada ya fainali ya Coupe de France ambapo PSG watacheza dhidi ya Angers Mei 27.

No comments:

Post a Comment