Tuesday, May 2, 2017

SHINJI KAGAWA APEWA OFA YA MKATABA MPYA DORTMUND.

MKURUGENZI wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amethibitisha kuwa Shinji Kagawa amepewa ofa ya mkataba mpya na klabu hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa katika kiwango bora katika kikosi cha Dortmund baada ya kuanza kwa kusuasua mapema mwanzoni mwa msimu. Dortmund wanaonekana kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na nyota huyo wa kimataifa wa Japan na watazungumza naye kuhusu kumuongeza mkataba mwingine kufuatia ule wa sasa kutarajiwa kumaliza mwakani. Akizungumzia kuhusu suala hilo, Zorc amesema watazungumza na Kagawa na wakala wake halafu wataona na uelekeo upi mazungumzo hayo yatakwenda. Kagawa ambaye alirejea kutoka Manchester United Agosti mwaka 2014 amefanikiwa kufunga mabao mawili na kusaidia mengine manne katika mechi tisa zilizopita za mashindano yote akiwa na Dortmund.

No comments:

Post a Comment