Tuesday, May 2, 2017

ROBBEN AFURAHIA KUFIKIA REKODI YA CRUYFF.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Arjen Robben amefanikiwa kufikia rekodi ya nguli wa zamani wa nchi hiyo Johan Cruyff ya kutwaa mataji 10 ya ligi, kufuatia Bayern Munich kutwaa taji lake la tano mfululizo la Bundesliga mwishoni mwa wiki iliyopita. Baada ya Bayern kujihakikishia kutwaa taji hilo kwa ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Wolfsburg, Robben aliwaambia wanahabari aliokuwa akizungumza nao kuwa amesikia amefikia rekodi ya nguli wa soka wa wakati wote wa Uholanzi. Robben amesema amefurahi kuona kuwa sasa yeye pamoja na Cruyff kwa pamoja wamewahi kutwaa mataji 10 ya ligi hivyo anajivunia sana mafanikio hayo. Robben mwenye umri wa miaka 33 jumla amewahi kushinda mataji sita ya Bundesliga akiwa na Dortmund, mawili na Chelsea, moja la La Liga akiwa na Real Madrid na lingine la Ligi Kuu ya Uholanzi.

No comments:

Post a Comment