Tuesday, May 2, 2017

FALCAO KUBAKI MONACO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Monaco, Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, la Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa na mafanikio makubwa Monaco toka arejee baada ya kushindwa kufanikiwa alipopelekwa kwa mkopo Manchester United na Chelsea. Toka msimu huu umeanza, Falcao amefanikiwa kufunga mabao 28 katika mechi 38 za mashindano yote akiwa na klabu hiyo. Ingawa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, Falcao anaonekana hana mpango wowote wa kuondoka Monaco. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na hilo, Falcao amesema anajisikia vizuri Monaco na familia yake tayari imeshazoea mazingira ya hapo hivyo hadhani kama atakwenda popote. Falcao mwenye umri wa miaka 31, anashika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa ligi msimu huu akiwa na mabao 19 nyuma ya Alexandre Lacazette mwenye mabao 24 na Edinson Cavani mwenye mabao 31.

No comments:

Post a Comment