Thursday, May 4, 2017

ILIBAKI KIDOGO NIMSAJILI MBAPPE - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa ilibaki kidogo amsajili Kylian Mbappe kutoka klabu ya Monaco mwaka jana. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, amekuwa akizivutia klabu mbalimbali toka apate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Monaco, akifunga mabao 24 katika mechi 39 alizoichezea timu hiyo msimu huu. Mbappe alikuwa tayari akiwindwa toka Machi mwaka 2016 wakati apovunja rekodi ya Thierry Henry ya kuwa mchezaji mdogo kabisa kuifungua bao Monaco katika mchezo dhidi ya Troyes na wakati huo Wenger alishaanza mchakato wa kumuwania. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na hilo, Wenger amesema ni kweli alijaribu kumsajili chipukizi huyo kwasababu alikuwa akikaribia kumaliza mkataba wake lakini Monaco walifanikiwa kumuongeza mkataba mwingine. Mbappe alikuwa sehemu ya kikosi cha Monaco kilichochabangwa mabao 2-0 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus jana.

No comments:

Post a Comment