Thursday, May 4, 2017

LUKE SHAW AONGEZA IDADI YA MAJERUHI MAN UNITED.

BEKI wa kuhsoto wa Manchester United, Luke Shaw anatarajiwa kukosa mechi zote zilizosalia msimu huu kutokana na kupata majeruhi ya mguu. Shaw mwenye umri wa miaka 21, anatarajia kuonwa na wataalamu ili kujua ukubwa wa tatizo lake baada ya Jumatatu kubainika kuwa alipata matatizo kwenye ngano ya goti lake. Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza alitolewa uwanjani baada ya kupita dakika tisa katika mchezo wa Jumapili iliyopita uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Swansea City huko Old Trafford. Mapema jana, akizungumza na wanahabari meneja wa United Jose Mourinho alithibitisha kuwa Shaw hatacheza tena msimu huu.

No comments:

Post a Comment