Thursday, May 4, 2017

RONALDO AWA MWANAMICHEZO WA KWANZA KUFIKISHA FOLLOWERS 100 INSTAGRAM.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameendelea kung’ara ndani na nje ya uwanja kutokana na umahiri wake mkubwa katika soka. Juzi nyota huyo shindig wa tuzo ya Ballon d’Or aliisaidia Madrid kupiga hatua moja kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Atletico Madrid katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Nyota huyo hakuishia hapo kwani ameendelea kuweka historia hata nje ya uwanja kwa kuwa mwanamichezo wa kwanza kufikisha mashabiki milioni 100 wanaomfuatilia katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram. Ronaldo amewaacha mbali wanamichezo wengine akiwemo hasimu wake wa karibu Lionel Messi wa Barcelona ambaye yeye anafuatiliwa na watu milioni 70.8 katika mtandao huo. Wachezaji soka ndio wanaongoza orodha za juu kwa kufuatiliwa Instagram, ambapo baada ya Ronaldo na Messi anayefuatia ni nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, huku nyota wa mpira wa kikapuu NBA LeBron James naye akiwepo kwenye top 10.

No comments:

Post a Comment