Thursday, May 4, 2017

KOEMAN ATAMANI KUINOA BARCELONA.

MENEJA wa Everton, Ronald Koeman amedai kuwa bado ana ndoto za kuja kuinoa Barcelona siku za usoni. Hata hivyo, beki huyo wa zamani ambaye alicheza kwa kipindi cha miaka sita Barcelona kuanzia mwaka 1989 mpaka 1995, amesema kwasasa anataka nguvu amezielekeza kwa Everton ili waweze kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Koeman mwenye umri wa miaka 54 yuko katika msimu wake wa kwanza kati ya mitatu aliyosaini kwenye mkataba wake kiangazi mwaka jana akitokea Southampton. Meneja huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea Camp Nou baada ya Lus Enrique kuweka wazi kuwa atajiuzulu nafasi yake hiyo mwishoni mwa msimu huu. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Koeman raia wa Uholanzi amesema anafurahi kuona watu wakimfikiria kwani wote wanafahamu kuwa yeye ni Barcelona. Koeman aliendelea kudai kuwa katika maisha yake ana ndoto mbili za kutimiza mojawapo ni kuinoa timu ya taifa ya nchi yake nafasi ambayo ameikosa kutokana na majukumu aliyonayo Everton na lingine ya kuinoa Barcelona siku zijazo.

No comments:

Post a Comment