Friday, May 5, 2017

MOURINHO KUWAPUMZISHA NYOTA WAKE MCHEZO DHIDI YA ARSENAL.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema atawapumzisha wachezaji wake katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal Jumapili hii. Ushindi wa bao 1-0 waliopata United katika mchezo wao wa nusu fainali ya mkondo wa kwanza ya Europa League dhidi ya Celta Vigo jana, unakuwa mchezo wao wa 10 kucheza toka Aprili mosi. Kufuatia United kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi, michuano ya Europa League inaweza kuwapa nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Akizungumza na wanahabari, Mourinho amesema wachezaji ambao wamecheza mechi nyingi hatawatumia katika mchezo wao wa Jumapili hii. Kama United wakifanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Stockholm Mei 24, utakuwa ni mchezo wao wa 64 msimu huu.

No comments:

Post a Comment