Friday, May 5, 2017

MOYES KUSHUKA NA SUNDERLAND.

MENEJA wa Sunderland, David Moyes amesema ataendelea kuinoa klabu hiyo msimu ujao pamoja na kushuka daraja. Sunderland wamekuwa na msimu mbaya, kufuatia kufanikiwa kushinda mechi tano pekee hivyo kujikuta wakishuka daraja huku kukiwa kumebaki mechi nne ligi kumalizika. Akizungumza na wanahabari, Moyes amesema anafahamu ni jambo gani la kufanya ili kuhakikisha wanarejea katika Ligi Kuu. Meneja huyo raia wa Scotland pia amesema mshambuliaji Jermain Defoe ambaye amefunga mabao 14 msimu huu, anaweza kuondoka.

No comments:

Post a Comment