Monday, April 17, 2017

WES MORGAN AREJEA KUIOKOA LEICESTER.

NAHODHA wa Leicester City, Wes Morgan amefanya mazoezi na wachezaji wenzake mapema leo wakati wakijiandaa na mchezo wao wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. Morgan alikosa mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika Vicente Calderon kufuatia kusumbuliwa na maumivu ya mgongo ambapo Leicester walifungwa bao 1-0. Hata hivyo, klabu hiyo ina matumaini kuwa beki huyo atarejea katika mchezo wa kesho, haswa kutokana na klabu hiyo kukumbwa na matatizo kwenye safu yao ya ushambuliaji. Robert Huth anatumikia adhabu na Younes Benalouane aliumia katika mchezo dhidi ya Crystal Palace Jumamosi iliyopita jambo ambalo linamfanya meneja Craig Shakespeare kupata wakati mgumu kwenye safu yake ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment