Thursday, June 1, 2017

AJAX YAIMARISHA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI.

KLABU ya Ajax Amsterdam imetangaza kukamilisha usajili wa Klaas-Jan Huntelaar na kumpa mkataba wa mwaka mmoja. Mshambuliaji huyo mkongwe alikuwa huru baada ya kuondoka Schalke 04 mwishoni mwa msimu huu na sasa amerejea tena Asterdam Arena. Ajax walikuwa wakitaka kuongeza mshambuliaji mwingine ili kusaidiana na mshambuliaji wao kiongozi Kasper Dolberg. Huntelaar mwenye umri wa miaka 33 aliwahi kuichezea Ajax mwaka 2006 mpaka 2008 na kufanikiwa kufunga mabao 105 katika mechi 136 za mashindano yote. Baada ya kutoka Ajax, Huntelaar amewahi kuzitumikia Real Madrid, AC Milan na Schalke.

No comments:

Post a Comment