KLABU ya Atletico Madrid imepoteza rufani yao waliyokata katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu ya kuzuiwa kusajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Hatua hiyo sasa inamaanisha kuwa klabu hiyo haitaruhusiwa kusajili mpaka itakapofika usajili wa dirisha doko Januari mwaka 2018. Atletico na mahasimu wao wa jiji Real Madrid walifungiwa kusajili kwa vipindi viwili vya usajili kwa kosa la kukiuka sheria ya usajili wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya miaka 18. Baada ya kushindwa rufani yao FIFA, Atletico walitumikia adhabu ya kutosajili katika dirisha la Januari mwaka huu kabla ya kuamua kukata rufani CAS. Kutokana na matokeo ya rufani yao Atletico sasa watakuwa wameshindwa kufanya usajili wowote kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment