Thursday, June 1, 2017

MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA PILI.

KLABU ya Manchester City imefanikiwa kufanya usajili wake wa pili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi kwa kukamilisha uhamisho wa kipa wa Benfica Ederson. Usajili huo unamfanya kipa huyo wa kimataifa wa Brazil kuwa mchezaji wa pili wa bafasi yake kusajili kwa fedha nyingi katika historia. Ederson mwenye umri wa miaka 23 ameigharimu City kitita cha paundi milioni 35 na kumfanya kuwa kipa wa pili ghali katika historia baada ya Gianliugi Buffon aliposajili kwenda Juventus akitokea Parma mwaka 2001. Ederson alisafiri kwenda Manchester Jumatatu na Jumanne alitua katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu. City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo pia kutangaza kumnasa kiungo wa Monaco Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 Ijumaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment